Mashtaka hayo ni kuhusu Hunter Biden, kukosa kulipa kodi kwa wakati, na kumiliki bunduki, wakati akitumia dawa za kulevya kinyume cha sheria.
Mbunge wa Marekani James Comer, ambaye amekuwa akichunguza fedha za familia ya Biden, alisema makubaliano hayo, ni sawa na kumpendelea mshukiwa, na kutomchukulia hatua zinazofaa.
Katika chapisho la mtandao wa kijamii, Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump alitaja makubaliano hayo kama yasiyotoa adhabu ifaayo, hasa ikilinganishwa na mashtaka 37 ambayo Idara ya Sheria iliwasilisha dhidi ya mwanasiasa huyo wiki mbili zilizopita, kwa madai ya kutumia vibaya nyaraka za siri baada ya kuondoka mamlakani, mnamo mwezi Januari mwaka 2021.
Trump na Warepublican wengine walisema kuchukuliwa kwa hatua tofauti kwa kesi hizo mbili nyeti kisiasa, kunaashiria mfumo wa haki, wa pande mbili nchini Marekani, huku idara ya Sheria ikiwapendelea Wademokrat, na kufungua mashtaka makali ya jinai dhidi ya rais huyo wa zamani, wa chama cha Republican.
Kura za maoni za kitaifa zinaonyesha Trump anaongoza wawaniaji wengine wa tikiti ya Republikan, wanaotaka kumng’oa mamlakani Rais Biden katika uchaguzi wa kitaifa wa 2024.
Garland, ambaye aliteuliwa na Biden kama afisa mkuu wa utekelezaji wa sheria nchini, mara kwa mara amesema kuwa Idara ya Sheria anayoiongoza, inafanya kazi bila kuegemea kisiasa, na amesema hivyo ndivyo ilivyokuwa katika kuamua kuhusu matokeo ya uchunguzi wa miaka mitano dhidi ya Hunter Biden.
Forum