Kulingana na kesi iliyowasilishwa mahakamani siku ya Jumanne, Hunter Biden, mwenye umri wa miaka 53, ambaye kwa muda mrefu ametatizwa na uraibu wa mihadarati na uchunguzi wa shughuli zake za biashara nje ya nchi, atakubali mashtaka mawili ya makosa ya kukosa kulipa kwa wakati, kati ya mwaka 2017 na 2018, na kukubali kuwekwa katika hali ya uangalizi, maarufu probation.
Kwa kuongezea, nyaraka za mahakama zilionyesha kwamba Idara ya Sheria ilikubali kutomfungulia mashataka kuhusiana na ununuzi wake wa bunduki mnamo mwaka wa 2018 alipokuwa akitumia dawa za kulevya, ingawa alidai kwenye hati ya ununuzi kuwa hakuwa anatumia dawa hizo.
Makubaliano hayo yanamtaka Biden kusalia bila kutumia dawa kwa miaka miwili na akubali kutomiliki tena bunduki, lakini ni lazima yaidhinishwe na jaji.
Forum