Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 12:15

Mwanaharakati Mtanzania mtetezi wa wasichana ashinda tuzo ya UN


Rebeca Gyumi
Rebeca Gyumi

Akiwa na umri wa miaka 31, Rebeca Gyumi tayari anaorodha ya mafanikio ambayo mtu yeyote wa umri wake atapenda kujivunia.

Amefanikiwa kupinga mfumo wa sheria nchini Tanzania ambako ndiko aliko zaliwa na kukulia, na kushinda uamuzi wa kesi ya ukombozi wa kipekee ulitolewa na mahakama mwaka 2016 ambao umeongeza umri wa kuolewa kutoka miaka 14 hadi 18.

Baada ya ushindi huo alianzisha taasisi ambayo imekuwa ikitetea elimu kwa wasichana; ameshinda Tuzo ya Unicef ya malengo ya kimataifa na ametajwa mwanamke bora mwaka 2016 katika Gazeti la New Africa Magazine.

Tayari ameshawasili New York ambako amepokea Tuzo ya Haki za Binadamu 2018 iliyotolewa na Umoja wa Mataifa.

“Nilikuwa nimeshtuka sana. Nimeshtuka na kushtukizwa bila ya kujua kwamba ninafikiriwa kutunukiwa zawadi hiyo yenye hadhi ya juu,” ameliambia kituo cha habari cha CNN.

Gyumi alikuwa mtoto yeye mwenyewe wakati alipoanza kuona uonevu ukifanyika katika mazingira yake. Alikuwa na umri wa miaka 13 wakati baadhi ya wanafunzi wenzie wakilazimishwa kukatiza masomo kutokana na ujauzito na wakiozeshwa.

Akijitolea katika harakati za juhudi zilizoanzishwa na vijana katika umri wa miaka 20, alianza kugundua kuwa ni tatizo la kitaifa na siyo la mahali ambako ni nyumbani kwao Dodoma.

“Hili lilinitatiza sana kuwa umri wa wavulana kuowa ulikuwa ni miaka 18 lakini wasichana ni miaka 14,” amesema.

Hadi alipoingia chuo kikuu kusoma sheria ndipo alipogundua kuwepo Sheria ya ndoa ya mwaka 1971 na kuona uwezekano wa kuanzisha hoja ya kisheria kupinga sheria hiyo.

Mwaka 2016, akiwa na uzoefu wa miaka kadhaa katika fani ya uwanasheria , Gyumi na marafiki zake waliamua kufanya hilo la kuipinga sheria hiyo.

Walianza kushughulikia kesi ya kisheria kupinga sheria ya ndoa, wakikusanya ripoti kuthibitisha kuwa ndoa za utotoni za wasichana ni tatizo la kitaifa na ni kwa nini lazima lizuiliwe.

Kwa mujibu wa tafiti ya kitaifa ya mbadiliko ya idadi ya watu na afya ya 2015/16, wasichana wawili katika ya watano wanaolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18 ikiwa na ongezeko la asilimia 37 nchi nzima.

XS
SM
MD
LG