Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi nchini Tanzania Sagahutu alikamatwa hivi karibuni eneo la mpakani wilayani Ngara alipokuwa akielekea Burundi.
Akizungumzia tukio hilo Jumanne, ofisa uhamiaji mkoa wa Kagera Abdallah Tiwo alisema mtuhumiwa huyo amepelekwa makao makuu kwa ajili ya uchunguzi.
"Ni kweli alikuwa anashikiliwa na uhamiaji mkoa wa Kagera, ila sasa anaelekea Dar es Salaam makao makuu ya uhamiaji," alisema.