Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:12

Burundi yafafanua sababu za kuzuia chakula kutoka Rwanda


Wabunge wa Burundi wakisubiri Pierre Nkurunziza kuapishwa Agosti 20, 2015.
Wabunge wa Burundi wakisubiri Pierre Nkurunziza kuapishwa Agosti 20, 2015.

Burundi imesema kuwa ni sababu za kiusalama ndio zilizopelekea serikali yake kuzuia msaada wa vyakula ambavyo vilikuwa vimenunuliwa kutoka Rwanda.

Msemaji wa jeshi la polisi la Burundi Pierre Nkurinkiye ameikumbusha jumuiya ya kimataifa madai ya serikali ya Burundi dhidi ya Rwanda kutokana na nchi hiyo kuhusika katika uvunjifu wa amani nchini Burundi.

Nkurikiye amesisitiza kuwa ni hatua ya busara kuzuia mzigo huo kwa ajili ya usalama wa Burundi.

"Kila mtu anafamu watu na vitu mbalimbali vilivyotumika kutoka nchi ile, katika kuvuruga usalama wa nchi hii kuanzia mwaka wa 2015," alisema kamanda huyo.

Kuingizwa kwa silaha

Amesema mtakumbuka kuwa silaha nyingi na wahalifu walikuja na kuwauwa viongozi.

"Nadhani kama wewe ni mrundi mtu akikwambia kuwa ni hatua ya kiusalama unaelewa," amesema kamanda huyo.

Wakati huohuo Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) hapa nchini pomoja na kukiri kuwa uhusiano kati ya Burundi na shirika hilo ni mzuri.

WFP watafuta ufumbuzi

Amesema kutokana na Burundi kupiga marufuku lori zenye kusheheni misaada kutoka Rwanda hautapatiwa ufumbuzi, wao watalazimika kuchukuwa njia mbadala ya kupitia Kobero kwenye mpaka kati ya Burundi na Tanzania ambayo itagharimu dola za Kimarekani 35,000 katika usafirishaji wa misaada hiyo.

Mzozo wa kidiplomatia kati ya Burundi na Rwanda umepelekea nchi ya Burundi kupiga marufuku misaada ya vyakula vilivyonunuliwa na WFP katika ghala za Rwanda.

Msafara wa malori ya shirika hilo yameamrishwa kurudi nchini Rwanda Jumanne baada ya kuzuiliwa kwenye mpaka baina ya nchi hizo kwa siku kadhaa.

Burundi yakabiliwa na uhaba

Hatua hiyo ambayo inatajwa na serikali kama ya kiusalama imechukuliwa licha ya Burundi kukabiliwa na uhaba wa chakula katika siku hizi za karibuni.

Mwandhishi wa idhaa ya Kiswahili amerepoti kuwa msaada watani 300 za maharagwe tayari ulirudishwa nchini Rwanda kutoka mpaka wa Rwanda na Burundi.

Kwa jumla tani 508 za vyakula zilizokuwa zikitarajiwa kuingia nchini Burundi kwa ajili ya kupewa familia 12 ikiwa ni pamoja na wakimbizi kutoka nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo waliopewa hifadhi nchini Burundi, na warundi walioathiriwa na mabadiliko ya hali na nchi na hivyo kukabiliwa na njaa.

Mwakilishi Mkazi wa WFP

Nicole Jake mwakilishi mkaazi wa WFP ameiambia sauti ya amerika kuwa hawakuwa na wasiwasi pale msafara wa malori uliposimamishwa mpakani mwishoni mwa wiki iliyopita kwa sababu ni hali ya kawaida katika nchi zingine za ukanda huo za Kenya, Uganda na kwingine kwa ajili ya ukaguzi.Lakini baadaye waliambiwa kuwa ni kwa sababu za kiusalama.

Amesema si mara ya kwanza kwa lori zetu kusimamishwa kwenye vituo vya mpakani, hilo halikuwatia wasiwasi.

"Lakini baada ya kuona zinazuiliwa hadi jumamosi, tuanza kusikitika na kuuliza kwenye idara ya polisi, wizara ya mambo ya ndani na kwingine, na tukaambiwa kuwa ni haut ya kiusalama," Jake amesema.

Baada ya kuambiwa hivyo tuliona hakuna sababu ya kuhatarisha maisha ya madereva na usalama wa malori, hivyo tukawaka warudi kule walikotoka, amesema.


XS
SM
MD
LG