Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:50

Korea Kaskazini yawageuza Wamarekani nyenzo ya nyuklia


Wamarekani Otto Warmbier mwezi machi 16, 2016, kushoto, Kim Dong Chul Aprili 29, 2016 wakifishwa mahakamani Korea Kaskazini.
Wamarekani Otto Warmbier mwezi machi 16, 2016, kushoto, Kim Dong Chul Aprili 29, 2016 wakifishwa mahakamani Korea Kaskazini.

Kuachiliwa kwa Wamarekani watatu wanaoshikiliwa Korea Kaskazini kunaelekea kuwa ni jambo ambalo halitatokea siku za karibuni.

Wachambuzi wa siasa wanatabiri kuwa wakati Washington na Pyongyang wakikaribia katika ncha ya mgogoro unaozidi kukua juu ya vitisho vya nyuklia katika rasi ya Korea inawezekana raia hawa wa Marekani wasiachiliwe huru kwa siku za karibuni.

Kim Sang Duk

Mkorea-Mmarekani Kim Sang Duk, ambaye pia anajulikana kama Tony Kim, amekuwa raia wa tatu wa Marekani kukamatwa nchini Korea Kaskazini, wakati aliposhikiliwa Jumamosi katika Uwanja wa Kimataifa wa Pyongyang akijaribu kuondoka nchini.

Kim ambaye ana umri wa miaka 58 alikuwa anafundisha masomo ya uhasibu huko Chuo Kikuu cha Sayansi cha Pyongyang (PUST,) ambacho ni chuo binafsi kinachofadhiliwa na nchi nyingi za Magharibi zenye mafungamano na makundi ya kikristo (Evangelists) inayosaidia kuwaelimisha watoto wa familia zenye uwezo.

Balozi Nikki Haley

Balozi Nikki Haley
Balozi Nikki Haley

Nikki Haley, balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, amesema Jumatatu kwamba kukamtawa kwa Kim ni jaribio la serikali ya Kim Jong Un inayoelemewa kutafuta njia ya kutafuta makubaliano na Marekani juu ya suala la program zake za nyuklia na makombora.

Ubalozi wa Sweden Pyongyang umethibitisha kukamtwa kwa Kim lakini Korea Kaskazini haijamfungulia mashtaka ya wazi yoyote.

Chuo kikuu cha PUST

Afisa wa Chuo Kikuu cha PUST ameliambia Shirika la Habari la Reuters kwamba kukamatwa kwa Kim hakuna mahusiano yoyote na shughuli zake pale chuoni lakini inawezekana ikawa kunafungamana na shughuli zake za kujitolea nje ya chuo katika vituo vya yatima.

Chuo kikuu cha PUST Korea Kaskazini
Chuo kikuu cha PUST Korea Kaskazini

Huko nyuma Korea Kaskazini imewakamata wamishonari kadhaa kwa kukaidi katazo la kuhubiri ambalo linachukuliwa ni kosa la jinai dhidi ya serikali.

Aliyekuwa naibu waziri wa mambo ya nje, Nicholas Burns amesema, “North Korea imekuwa na historia ya kuwateka Wamarekani, kuwazuilia bila ya sheria na bila ya msingi wowote. Wanafanya hili bila shaka kwa ajili ya kuongeza dau kwa Marekani na kupata sababu ya kufanya mazungumzo na Marekani.

XS
SM
MD
LG