Msemaji wa idara ya kitaifa ya misitu, Aderienne Freeman, amesema kwamba moto mkubwa unaendela kuteketeza sehemu za Mckinney, katika msitu wa kitaifa wa Klamath, North Carolina.
Ukubwa wa moto huo umeongezeka na kuenea hadi umbali wa kilomita 207 mraba, siku mbili baada ya kuripotiwa katika kaunti ya Siskiyou, yenye idadi ndogo ya watu.
Uchunguzi unaendelea kubaini kilichosababisha moto huo.