Austin na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, wamehojiwa na kamati ya Senate inayosimamia matumizi ya fedha za serikali, kuhusu ombi la Rais Joe Biden la dola bilioni 106, kuisaidia Ukraine, Israel na kwa ajili ya usalama kwenye mipaka ya Marekani.
Austin amesisitiza kwamba endapo Marekani haingetoa msaada kwa Ukraine, Rais wa Russia Vladimir Putin angekuwa ameshafikia malengo yake nchini Ukraine, na kuongezea kwamba msaada zaidi kwa washirika wa Marekani ni muhimu sana kwa ajili ya usalama wa taifa.
Biden aliomba dola bilioni 61.4 kwa ajili ya Ukraine. Nusu ya pesa hizo zitatumika ndani ya Marekani kutengeneza silaha na kujaza pengo lililoachwa baada ya silaha hizo kutolewa kwa Ukraine katika msaada wa awali.
Baraza la wawakilishi limeidhinisha dola bilioni 113 kama msaada wa Ukraine tangu Russia ilipoivamia nchi hiyo kijeshi Februari 2022.
Forum