Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 22:15

Ukraine inasema watu 9 wa familia moja wameuawa katika mji unaokaliwa na Russia


Afisa wa polisi akisimama mbele ya jengo lililoharibiwa kufuatia shambulio la Russia katika mji wa Avdiivka, katika mkoa wa Donetsk, Oktoba 17, 2023.
Afisa wa polisi akisimama mbele ya jengo lililoharibiwa kufuatia shambulio la Russia katika mji wa Avdiivka, katika mkoa wa Donetsk, Oktoba 17, 2023.

Ukraine inasema familia ya watu tisa walipigwa risasi na kuuawa ndani ya nyumba yao katika mji wa mashariki wa Volnovakha unaokaliwa na Russia.

Picha za nyumba hiyo zilizotolewa na mamlaka zinaonyesha tukio la uhalifu wa kutisha, huku waathirika wakiwa wamekufa wamelala kwenye vitanda vyao na kuta zimejaa damu.

Ofisi ya mwendesha mashtaka inayoungwa mkono na Ukraine katika mkoa wa Donetsk ulipo mji wa Volnovokha, inasema mauaji hayo yalitokea baada ya mwenye nyumba kupinga ombi la kundi la watu waliovalia sare za kijeshi kuondoka ndani ya nyumba hiyo ili wanajeshi wa Russia wakae humo. Ofisi hiyo inasema watoto wawili ni miongoni mwa waliouawa.

Waendesha mashtaka wa Russia wanasema wanajeshi wawili kutoka eneo la mbali la mashariki mwa Russia wamezuiliwa kwa kuhusishwa na mauaji hayo.

Wanajeshi hao walisaini mkataba na jeshi la Russia kuhudumu nchini Ukraine.

Forum

XS
SM
MD
LG