Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 22:11

Russia yadai kutungua droni za Ukraine usiku kucha


Picha ya drone zinazotumika kwenye vita vya Russia na Ukraine
Picha ya drone zinazotumika kwenye vita vya Russia na Ukraine

Russia imesema Jumapili kwamba imetungua  droni 36 usiku kucha kwenye bahari ya Black Sea pamoja na Peninsula ya Crimea.

Ukraine ambayo imezidisha kampeni yake dhidi ya Russia haijasema lolote kuhusu shambulizi la usiku kucha. Katika mkutano nchini Japan Jumapili, mawaziri wa biashara wa G7 wametoa taarifa ya pamoja kuhusu uvamizi wa Russia nchini Ukraine wakiuita ni “ ni ukatili wenye uchokozi, hauna uhalali na uvamizi haramu wa kivita.

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema Jumapili kwamba vyuo vikuu vya Russia vimeamuriwa kusitisha masomo ya aina yoyote yenye majadiliano hasi kuhusu harakati za kisiasa, kiuchumi na mienendo ya kijamii kuhusu Russia. Wizara hiyo imesema kwamba hiyo ni hatua nyingine ya kuzuia kusambaa kwa taarifa wakati Russia ikiwa vitani, na kwamba ni vigumu sana kujadili kuhusu masuala ya sera hadharani.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy Jumamosi wakati wa hotuba yake ya kila siku kwa taifa amesema kwamba kongamano la Malta ambalo lilifanyika siku hiyo kwa kuwa pia ni ya maadhimisho ya Ukraine ya kumalizika kwa vita vya pili vya dunia, na pia maadhimisho ya kufukuzwa kwa wa Nazi kutoka katika eneo hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG