Kuahirishwa upya kwa kesi hii inamaanisha kuwa Ibrahim, mwenye miaka 30 raia wa Kenya, atakuwa ameweka kizuizini huko New York kwa takriban miaka mitatu wakati atakapojua muda wa kifungo chake. Kifungo hicho kinaweza kuwa kati ya miaka 10 hadi maisha.
Kaka yake Ibrahim, Baktash, alihukumiwa kifungo cha miaka 25 Agosti, 2019.
Dawn Cardi, wakili wa Ibrahim, amesema katika mahojiano Ijumaa kuwa kupangwa kusikilizwa kwa kesi hiyo katika mahakama ya serikali kuu huko Manhattan hakukuweza kufanyika kwa sababu mteja wake “anamaswali yasiyojibiwa” kuhusu kesi yake.
Chini ya sheria za mahakama za Marekani, hukumu haiwezi kuendelea kutolewa endapo mtuhumiwa au mhalifu aliyekiri makosa akimshawishi jaji kuwa haridhiki na utaratibu wa kisheria katika usikilizaji wa kesi kwani haukuwa unajitosheleza.
Katika taarifa iliyotumwa kwa Jaji Victor Marrero anayesikiliza kesi hiyo, Ibrahim Akasha amesema “amechanganyikiwa” na “yuko kizani” kwa sababu hakupata ufafanuzi wa suala lake la kisheria kutoka kwa Cardi.