Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 04:02

Milio ya risasi yasikika usiku kucha Port- au-Prince, Haiti


Ghasia kwenye mji mkuu wa Haiti wa Port-au-Prince.
Ghasia kwenye mji mkuu wa Haiti wa Port-au-Prince.

Milio ya risasi imesikika usiku wa kuamkia Jumamosi kwenye mji mkuu wa Haiti wa Port-au-Prince, mwanahabari wa AFP alieko huko amesema, huku wakazi wakiendelea kutafuta hifadhi, kufuatia kuzuka kwa  ghasia za magenge siku chache zilizopita chini humo.

Ripoti zinasema kwamba hali ya kibinadamu inaendelea kudorora, wakati mashirika yasiyo ya kiserikali yakionya kuhusu uhaba wa chakula na dawa, kwenye taifa hilo lililotatizika la Caribbean.

Kulingana na mwanahabari huyo wa AFP, aliyekuwa kwenye eneo la tukio, milio ya risasi ilisikika Ijumaa usiku, hasa kwenye maeneo la kusini magharibi mwa Port-au-Prince ya Turgeau, Pacot, Lalue na Canape-Vert.

Makundi ya magenge ambayo tayari yamechukua udhibiti wa sehemu kubwa ya Port au Prince pamoja barabara muhimu kuelekea kwenye sehemu nyingine za nchi, pia yameshambulia maeneo muhimu ya serikali katika siku za karibuni, zikiwemo jela ambako wengi wa wafungwa 3,800 wametoroka.

Magenge hayo pamoja na baadhi ya raia wanaitisha kujiuzulu kwa waziri mkuu Ariel Henry, aliehitajika kuondoka madarakani mwezi uliopita, lakini badala yake akakubaliana kugawana madaraka na upinzani, hadi uchaguzi mpya ufanyike.

Forum

XS
SM
MD
LG