Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 13:44

Mfumo wa ulinzi wa anga wa Russia watungua droni 83 zilizotumwa na Ukraine


Rais wa Russia Vladimir Putin
Rais wa Russia Vladimir Putin

Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema kwamba mfumo wake wa ulinzi umetungua ndege zisizokuwa na rubani 83 kutoka Ukraine, katika mikoa sita, mapema leo Novemba 1.

Taarifa ya wizara hiyo iliyochapishwa kwenye ukurasa wa Telegram inasema kwamba ndege zisizokuwa na rubani 36 zimeangushwa katika mkoa wa Kursk, 20 Byyansk, 12 katika Crimea, nane zimeangushwa Voronezh, nne Oryol na tatu katika Belgorod.

Mikoa ya Ukraine iliyogawanyika chini ya uvamizi wa Russia.
Mikoa ya Ukraine iliyogawanyika chini ya uvamizi wa Russia.

Gavana wa Byransk amesema kwamba mtu mmoja amejeruhiwa katika shambulizi la ndege isiyokuwa na rubani ya Ukraine dhidi ya jengo lenye makazi ya watu katika mji wa Bryansk.

Katika tukio jingine, ndege isiyokuwa na rubani imeangukia gala la mafuta katika mji wa Svetlograd.

Na katika bandari ya Odesa, kombora la Russia limepiga kituo cha wazima moto na kujeruhi wazima moto wawili.

Vyanzo vya habari hii ni RFE/RL

Forum

XS
SM
MD
LG