Vikosi vya kijeshi vya Korea Kaskazini vimepelekwa katika eneo la mpaka la Russia la Kursk, idara ya ujasusi ya kijeshi ya Ukraine ilisema Alhamisi. Kursk ilikuwa sehemu ya uvamizi mkubwa wa Ukraine msimu huu wa joto.
Vikosi vya kwanza vya kijeshi kutoka Korea, ambavyo vilifunzwa katika uwanja wa mafunzo wa mashariki mwa Russia, tayari vimefika katika eneo la mapigano la vita vya Russia na Ukraine hasa Oktoba 23, 2024, kuwepo kwao kulirekodiwa katika mkoa wa Kursk idara ya ujasusi ilisema katika taarifa.
Idara ya ujasusi ilisema takriban wanajeshi 12,000 wa Korea Kaskazini, wakiwemo maafisa 500 na majenerali watatu, wanapatiwa mafunzo katika kambi tano za kijeshi za Russia.
Forum