Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 13:06

Makombora zaidi yamepiga Ukraine


Nyumba iliyoharibiwa na kombora la Russia, mjini Kyiv, Ukraine Oct 26 2024 Picha: Reuters
Nyumba iliyoharibiwa na kombora la Russia, mjini Kyiv, Ukraine Oct 26 2024 Picha: Reuters

Makombora ya Russia yameua watu watatu akiwemo mtoto katika mji wa Dnipro nchini Ukraine, huku kijana na mtu mwingine mmoja wameuawa mjini Kyiv na katika mkoa ulio karibu, maafisa wamesema Jumamosi.

Gavana wa mkoa wa Dnipropetrovsk, Sergiy Lysak amesema mashambulizi hayo ya leo usiku katika mji wa Dnipro yamejwaeruhi watu 19 na kuharibu majengo kadhaa.

Jengo la ghorofa mbili lenye makazi ya watu liliharibiwa, amesema.

Mashambulizi mengine katika mji mkuu wa Kyiv na sehemu za karibu yamesababisha vifo vya watu wawili, akiwemo msichana aliyeuawa n shambulizi la ndege zisizokuwa na rubani.

Mashambulizi ya makombora na ndege zisizokuwa na rubani za Russia yameongezeka katika mjini Kyiv huku utawala wa Ukraine ukiomba msaada zaidi wa mfumo wa ulinzi wa anga kukabiliana na mashambulizi hayo.

Forum

XS
SM
MD
LG