Elliot Broidy alifunguliwa mashtaka katika mahakama ya serikali kuu Washington kwa kosa moja la njama kwa kitendo cha kuwa wakati wa kigeni aliyekuwa hajasajiliwa baada ya madai ya kuwa alikubali kupokea mabilioni ya dola za Marekani kwa ajili kuushawishi utawala wa Trump.
Mashtaka hayo yaliotangazwa kwa umma Alhamisi, yamesema Broidy alipewa shughuli hiyo mwaka 2017 na raia wa kigeni ambaye hajatajwa jina lake, anayefahamika ni raia wa Malaysia Low Taek Jho, kuwashinikiza maafisa wa Marekani kumaliza uchunguzi wao kwa kashfa inayomuandama waziri mkuu wa Malaysia wa wakati huo Najib Razak.
Kashfa hiyo ilihusisha wizi wa zaidi ya dola za Marekani bilioni 4.5 kutoka mfuko wa kitega uchumi wa 1MDB, na Low alishutumiwa kuwa kiini katika kuhamisha na kuficha fedha hizo zilizokuwa zimeibiwa.
Wakati huo Broidy alikuwa naibu mwenyekiti wa fedha wa taifa wa Kamati ya Taifa ya Chama cha Republikan baada ya kuwa mchangishaji mkuu wa kampeni ya Trump 2016 ya kuwania urais iliyokuwa na mafanikio.
Baada ya kuajiriwa na Low, Broidy yeye binafsi alimwambia Trump amkaribishe Najib kucheza golf wakati kiongozi huyo wa Malaysia alipozuru Marekani Septemba 2017, mashtaka hayo yameeleza.
Lengo ilikuwa ni kumpa nafasi Najib “ kujaribu kutatua suala la kashfa ya 1MBD” akiwa na kiongozi wa Marekani, nyaraka hiyo imeeleza.
Mchezo huo wa golf haukufanyika, na Low alishtakiwa mwaka 2018 kwa kuhusika kuiba mabilioni kutoka kitenga uchumi cha 1MBD.
Low, ambaye pia amefunguliwa mashtaka Malaysia juu ya kashfa hiyo, amerejea kukanusha hakufanya kosa lolote. Pia haijulikana mahali alipo.
Pia, mwezi Mei 2017 Low alimtambulisha Broidy kwa waziri wa China, na walizungumzia utashi wa Beijing wa kuitaka Washington kumsafirisha mfanyabiashara wa China, mashtaka hayo yameeleza.
Haikutaja jina lolote, lakini mfanyabiashara huyo anajulikana kuwa ni Guo Wengui, ni mfanyabiashara mpinzani maarufu wa serikali.
Kwa mujibu wa jarida la Wall Street, afisa huyo wa China alikuwa Sun Lijun, wakati huo akiwa waziri mdogo usalama wa umma mwenye mamlaka makubwa China.
Mashtaka hayo yanaeleza ushawishi wa nguvu wa Broidy kwa White House, idara ya sheria na vyombo vya usalama kwa niaba ya China, ikiwemo mawasiliano na lakini sio mazungumzo ya moja kwa moja na Trump.
Lengo la udanganyifu katika ushawishi huu, mashtaka hayo yameeleza, ilikuwa “kutengeneza mamilioni ya dola za Marekani kwa kumwezesha Broidy na kufanyika ushawishi kwa rais na utawala wake.”
Mashtaka haya yamekuja wiki kadhaa baada ya mshirika mkuu wa Low na Broidy, mfanyabiashara mwanamke Nickie Mali Lum Davis, kukiri mashtaka ya kufanya ushawishi kinyume cha sheria katika kesi ya 1MDB na kesi ya Guo.
Guo amebakia Marekani, ambako ameendelea kufanya kampeni dhidi ya mamlaka za Beijing, akishirikiana karibu na mshirika wa muda mrefu wa Trump, Steve Bannon.
Bannon alikamatwa mwezi August wakati akiwa katika boti ya Guo nje ya pwani ya Connecticut na kufunguliwa mashtaka ya ulaghai wa fedha za michango kwa ajili ya mradi wa ukuta kmpaka wa Mexico.