Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:21

Jaji abatilisha amri ya Gavana wa Texas ya vituo vya kupokea kura

Wafanyakazi wakiandaa nyaraka za kupiga kura Septemba 3, 2020 kuzituma kwa njia ya posta kwa ajili ya wanaopiga kura mapema.

Uamuzi wa jaji wa serikali kuu unamaanisha kuwa wapiga kura katika jimbo la Texas Marekani watakuwa na sehemu kadhaa zilizotengwa ambazo wataweza kupeleka kura zao wanazopiga mapema kwa ajili ya uchaguzi wa rais Novemba.

Jaji wa Wilaya Marekani Robert Pitman ametoa ruhusa Ijumaa dhidi ya amri ya Gavana wa Texas Greg Abbott ya kuweka kituo kimoja tu kila kaunti cha kupokea kura zinazopigwa mapema.

Abbott, Mrepublikan, alisema kuwa kupunguza idadi ya vituo vya kupokea kura ilikuwa kwa ajili ya kuzuia wizi wa kura. Amri hiyo aliitolewa baada ya zoezi hilo la watu kuwasilisha kura zao mapema katika masanduku kuwa limekwisha anza.

Pitman ameandika katika uamuzi wa kurasa 46, “Kwa kupunguza vituo vya watu kuacha kura zao za mapema wanazopiga katika kituo kimoja kwa kila kaunti, wapiga kura wazee na walemavu wanaoishi katika kaunti kubwa na zilizo na watu wengi huko Texas ni lazima wasafiri masafa marefu kufika kwenye vituo vya kuacha kura vilivyo na msongamano wa watu, ambako watakuwa katika hatari ya kuambukizwa virusi vya corona kwa sababu tu ya kutekeleza haki yao ya kupiga kura na ili ziweze kuingizwa katika hesabu.”

Wanaharakati wanaotetea haki ya kupiga kura wamedai kuwa uamuzi wa Abbot ulikuwa unakusudia kukandamiza upigaji kura.

Marekani inayo historia ya muda mrefu kupiga yaupigaji kura wa mapema, lakini mwaka huu Rais Mrepublikan Donald Trump na Wabunge wa Republikan wamepinga hilo kwa nguvu zote.

Haijajulikana mara moja iwapo Abbott atakata rufaa juu ya uamuzi huo.

Uamuzi wa jaji wa serikali kuu unamaanisha kuwa wapiga kura katika jimbo la Texas Marekani watakuwa na sehemu kadhaa zilizotengwa ambazo wataweza kupeleka kura zao wanazopiga mapema kwa ajili ya uchaguzi wa rais Novemba.

Jaji wa Wilaya Marekani Robert Pitman ametoa ruhusa Ijumaa dhidi ya amri ya Gavana wa Texas Greg Abbott ya kuweka kituo kimoja tu kila kaunti cha kupokea kura zinazopigwa mapema.

Abbot, Mrepublikan, alisema kuwa kupunguza idadi ya vituo vya kupokea kura ilikuwa kwa ajili ya kuzuia wizi wa kura. Amri hiyo aliitolewa baada ya zoezi hilo la watu kuwasilisha kura zao mapema katika masanduku kuwa limekwisha anza.

XS
SM
MD
LG