Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 16:39

Mawaziri wa Afya wa SADC kukutana kujadili changamoto za Mpox


Wagonjwa wakimsikiliza daktari nje ya kituo kinachotoa matibabu ya Mpox huko Goma Kaskazini, DRC Agosti 17, 2024. Picha na AFP
Wagonjwa wakimsikiliza daktari nje ya kituo kinachotoa matibabu ya Mpox huko Goma Kaskazini, DRC Agosti 17, 2024. Picha na AFP

Mkutano wa 44 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika uliofanyika Harare, Zimbabwe umemalizika huku viongozi wakijadili changamoto zinazolikabili bara hilo , ikiwa ni pamoja na mpox.

Katibu Mtendaji wa SADC Elias Magosi amesema mkutano wa mawaziri wa afya utaitishwa “kuwezesha utaratibu wa kukabiliana na ugonjwa huo, ambao umeenea katika zaidi ya nchi kumi za Afrika.

Mkutano wa viongozi nchi za jumuiya hiyo ulianza Jumamosi, ambapo Magosi, alitoa “mshikamano na uungaji mkono” kwa wajumbe wa mataifa wanachana walioathiriwa na mpox na kuliomba shirika la Afya Duniani, vituo vya Afrika vya kudhibiti magonjwa na washirika kukabiliana na ugonjwa huo

Wiki hii WHO ilitangaza mlipuko wa mpox Afrika kuwa dharura ya afya duniani.

Katika kanda ya SADC ikiwemo Congo, ambayo ina zaidi ya asilimia 90 ya visa vya mpox.

Wanasayansi pia wametambua aina mpya ya mpox huko Congo ambayo inaweza kuwa na uwezo wa kuambukiza zaidi

WHO imekuwa na wasiwasi wa kusambaa zaidi katika mipaka ya kimataifa , na Sweden imeripoti kisa chake cha kwanza cha kirusi kipya cha mpox.

Forum

XS
SM
MD
LG