Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 14:42

Mawakili wa Trump kuwasilisha utetezi katika siku moja

Kutoka kushoto : David Schoen, Bruce Castor na Michael van der Veen, mawakili wa Rais wa zamani Donald Trump, wakiwasili Bungeni siku ya tatu ya kesi ya kufunguliwa Trump mashtaka ya uchochezi kwa mara pili katika Baraza la Seneti, Alhamisi Feb 11, 2021, Washington, (AP Photo/Jos

Mawakili wa Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump wanasema wanahitaji siku moja tu kuwasilisha kesi ya mteja wao ambaye anakabiliwa na mashtaka kwenye baraza la Seneti la Marekani.

Mawakili wa Trump watatoa utetezi wa rais huyo wa zamani Ijumaa bila ushahidi wowote wa moja kwa moja kutoka kwake kwani amekataa kushiriki katika kesi hiyo.

Utetezi unafuatia siku mbili za uwasilishaji wa mashtaka uliofanywa na Wademocrat katika Bunge wanaohusisha matamshi ya Trump kwenye mkutano wa Januari 6 na vitendo vya genge la wafuasi wake waliovamia jengo la bunge la Marekani muda mfupi baadaye katika jaribio la kuzuia urasmishaji wa matokeo ya uchaguzi wa rais wa mwaka 2020.

Katika hatua isiyo ya kawaida Alhamisi, Maseneta watatu wa Republican Lindsey Graham wa South Carolina, Ted Cruz wa Texas na Mike Lee wa Utah ambao ni wasimamizi katika kesi hiyo, walikutana na mawakili wa Trump.

Kituo cha televisheni cha CNN kimeripoti kwamba David Schoen, mmoja wa mawakili wa Trump, alisema wabunge hao walitaka kuhakikisha kuwa timu ya utetezi ya Trump ilikuwa inajua utaratibu kabla ya uwasilishaji wa utetezi Ijumaa

XS
SM
MD
LG