Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 22:52

Matumaini ya kuwapata walionusurika ajali ya bwawa la patel yafifia


Maafisa wa jeshi wakiondoa maji kutoka katika bwawa la jirani kuepusha mafuriko mengine, baada ya bwawa la Patel liliopo katika eneo la Solai, Kaunti ya Nakuru, Kenya, kupasuka na kusababisha mafuriko Mei 11, 2018.
Maafisa wa jeshi wakiondoa maji kutoka katika bwawa la jirani kuepusha mafuriko mengine, baada ya bwawa la Patel liliopo katika eneo la Solai, Kaunti ya Nakuru, Kenya, kupasuka na kusababisha mafuriko Mei 11, 2018.

Zoezi la kuwatafuta watu waliopotea baada ya Bwawa la Patel lilioko eneo la Solai, kaunti ya Nakuru, kupasuka zinaendelea nchini Kenya. Zaidi ya watu 40 wamepoteza maisha kufuatia kupasuka kwa bwawa hilo.

Wiki kadhaa za mvua kubwa zimesababisha mafuriko na mmomonyoko wa udongo kote nchini na kusababisha vifo vya watu 175.

Jumatano bwawa hilo kubwa linalotumika kwa umwagiliaji huko Solai takriban kilomita 40 kaskazini mwa Nakuru Kenya, kwenye jimbo la Rift Valley lilipasuka na kusababisha maji kubomoa nyumba za watu na maeneo mengine ya biashara .

Gavana wa Nakuru Lee Kinyanjui amesema miili ya watu 44 imepatikana na ameonya kuwa bwawa jingine lililoko ndani ya eneo hilo litabomolewa ili kuepuka janga kama hilo kutokea. Maelfu ya watu walipelekwa katika hospitali kufuatilia janga hilo.

Mwandishi wa VOA ameripoti kuwa huduma za dharura za uokozi zinawashirikisha watu waliojitolea ambao wanaendelea kufukua matope kwa kutumia mikono.

Hata hivyo juhudi zao zilikatishwa na mvua kubwa zilizonyesha Alhamisi na kusababisha zoezi la uokozi kuanza tena leo.

XS
SM
MD
LG