Manusura wa mafuriko hayo wameeleza kuwa maji yameharibu nyumba na maeneo ya biashara baada ya Bwawa la Patel kupasuka katika kitongoji cha Solai, takriban kilomita 150 kaskazini magharibi mwa mji wa Nairobi.
Maafisa wa serikali wamesema kuwa watu zaidi ya 40 wameokolowa na kupelekwa hospitali, na timu za waokoaji zinaendelea kuwatafuta waathirika wengine Alhamisi ambao huenda wamekwama katika baadhi ya maeneo yaliokumbwa na mafuriko.
Eneo hilo limeshuhudia mvua kubwa katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, zilizosababisha mafuriko na mmomonyoko wa udongo ambazo tayari yalikuwa yameuwa watu zaidi ya 130.
Serikali ya Kenya imesema Jumatano kuwa mvua hizo zimesababisha watu 220,000 kuhama makazi yao.