Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 03:19

Kenya yachukua tahadhari kufuatia mlipuko wa Ebola DRC


Uwanja wa ndege wa kimataifa Jomo Kenyatta Nairobi, Kenya
Uwanja wa ndege wa kimataifa Jomo Kenyatta Nairobi, Kenya

Serikali ya Kenya imechukua tahadhari katika uwanja wake wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) na maeneo ya mipakani baada ya ugonjwa wa Ebola kuripotiwa kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Wizara ya Afya nchini DRC imethibitisha kuwepo kwa wagonjwa wawili wenye ugonjwa huo.

Watu 17 walikuwa wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na ugonjwa usiojulikana huko DRC na unadhaniwa kuwa ni Ebola.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Kenya Waziri wa Afya Sicily Kariuki amesema kuwa kuanzia sasa wasafiri wote wanaowasili uwanja wa ndege wa JKIA na maeneo mengine ya mpakani nchini Kenya ikiwemo Busia na Malaba watapimwa viwango vya joto mwilini kwa kuchukua tahadhari.

“Katika maeneo haya, kumewekwa vifaa vya kuwagundua watu ambao viwango vyao vya joto viko juu,” amesema.

Wakati huohuo Nigeria pia imeanza kuchukua tahadhari dhidi ya maradhi hayo kwa kuweka uangalizi mkali katika mipaka yake.

Wataalam wa maradhi ya Ebola kutoka wizara ya afya nchini DRC watajumuika na wale wa shirika la afya duniani WHO kwenda jimbo la Equateur baada ya kupokea taarifa za kuwepo ugonjwa huo.

Mnamo mwaka 2014 watu zaidi ya 11,000 walipoteza maisha nchini Guinea, Sierra Leone na Liberia.

Matokeo ya uchunguzi wa maabara uliofanyika kuthibitisha matukio mawili ya Ebola kati ya sampuli tano zilizochukuliwa (2014) kutoka kwa wagonjwa waliokuwa wakishukiwa kuwa na virusi hivyo zilipelekea Shirika la afya duniani (WHO) kutoa tangazo hilo.

XS
SM
MD
LG