Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 21:21

Matokeo ya awali uchaguzi wa rais Kenya yaonyesha ushindani ni mkali


Maafisa wa uchaguzi wakihesabu kura katika kituo cha kupiga kura cha Shule ya Msingi ya Kilimera, Nairobi, Kenya, Aug. 9, 2022.
Maafisa wa uchaguzi wakihesabu kura katika kituo cha kupiga kura cha Shule ya Msingi ya Kilimera, Nairobi, Kenya, Aug. 9, 2022.

Zaidi ya vituo vya kupigia kura 43,000 vimewasilisha matokeo yao ya uchaguzi wa rais kutokana na kura zilizopigwa Jumanne. Matokeo ya awali yanaonyesha ushindani mkali kati ya wagombea wawili wakuu wa uchaguzi wa urais.

Matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais yanaonyesha ushindani mkali kati ya wagombea wakuu wawili, Raila Odinga na William Ruto.

Hadi kufikia saa saa tatu asubuhi kwa saa za Kenya, vituo vya kupiga kura 43,615 kati ya 46,229 vilikuwa vimewasilisha matokeo ya uchaguzi wa urais yakisubiri kuthibitishwa kabla ya kutangazwa kwa umma.

Kila mgombea alikuwa amepata kura milioni 1.2 hadi kufikia saa tatu asubuhi, kulingana na vyombo vya habari vya Kenya. Matokeo bado yanaendelea kuhesabiwa.

Tume inatarajiwa kuanza kuthibitiha matokeo baada ya maafisa wa uchaguzi kuripoti katika makao makuu ya tume ya uchaguzi Nairobi.

Tume itatangaza matokeo rasmi ya mwisho ya uchaguzi wa urais baada ya kuthibitisha fomu 46,229 zilizowasilishwa kutoka katika vituo vya kupiga kura kote nchini. Kuthibitishwa kwa matokeo haya kunaweza kuchukua siku kadhaa.

Tume ya uchaguzi inasema inaamini Wakenya milioni 13.2 wamepiga kura.

Hiyo ni asilimia 60 ya wapiga kura waliosajiliwa.Katika uchaguzi wa mwaka 2017, takriban asilimia 80 ya waliojiandikisha walipiga kura.

Idadi ya ndogo ya waliojitokeza inalauiwa kutokana na ufisadi ulikothiri na kushindwa kwa viongozi wa kisiasa kutekeleza ahadi za maendeleo ya kisiasa, kijamii na kiuchumi wanazotoa katika kila uchaguzi.

XS
SM
MD
LG