Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 10:07

IEBC: Tutaanza kutangaza matokeo baada tu ya kuhakikisha kwamba ndio yaliyotangazwa kwenye vituo vya kupigia kura.


Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati (katikati),akihutubia waandishi wa habari katika ukumbi wa Bomas Nairobi, Kenya, Oct. 25, 2017.
Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati (katikati),akihutubia waandishi wa habari katika ukumbi wa Bomas Nairobi, Kenya, Oct. 25, 2017.

Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka ya Kenya IEBC Wafula Chebukati, amesema kwamba matokeo ya kura yaliyotangazwa kwenye vituo vya kupigia kura ndiyo ya mwisho, na kwamba hayawezi kubadilishwa na mtu yeyote.

Katika hotuba yake kwa waandishi wa habari katika ukumbi wa Bomas (saa nne usiku), Chebukati amesema kwamba upigaji kura umemalizika katika vituo vingi, japo unaendelea katika vituo ambavyo vilichelewa kufungua.

"Upigaji kura unaendelea Kakamega, Makueni, Isiolo na katika baadhi ya sehemu za Nairobi ambako vituo vilichelewa kufunguliwa.” Amesema Chebukati akiongezea kwamba "hapa Bomas, tunachofanya ni kuhakiki tu kwamba fomu tulizopokea kutoka katika kila kituo ni za kweli. Sheria inaitaka IEBC kuhakiki fomu 34A inazopokea na kutangaza mshindi ndani ya muda wa siku 7.”

Amesema kwamba vituo 26,881 kati ya 46,229 kote nchini vimemaliza kuhesabu kura na kutuma fomu zake hadi Bomas.

"Tume itaanza kutangaza matokeo itakapomaliza kuhakikisha kwamba matokeo hayo ni kweli.”

XS
SM
MD
LG