Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 15:15

Marekani yarekodi mashambulizi 38 ya risasi kwa raia, watu wanne wauawa mwanzoni mwa 2023

Polisi wakifanya msako katika nyumba iliyoko jirani baada ya mtu mwenye bunduki kufyatua risasi na kujeruhi wanafunzi watatu wa Chuo wenye asili ya Kipalestina huko Burlington, Vermont, Marekani Novemba 25, 2023. Picha kwa hisani ya Wayne Savage via REUTERS.

Marekani imerekodi  mashambulizi 38 ya risasi kwa raia, ambapo takriban watu wanne waliuawa, tangu mwanzoni mwa 2023, idadi kubwa zaidi tangu 2006, kulingana na ripoti mbili za Washington Post zilizochapishwa Jumatatu.

Ripoti hizo, zikinukuu data kutoka hifadhi ya data ya mauaji ya watu iliyokusanywa na USA Today, Associated Press na Chuo Kikuu cha North Eastern, zikisema kwamba visa viwili vya ufyatuaji risasi huko Texas na Washington katika chini ya dakika 90 Jumapili alasiri viliiweka nchi kwenye "hatua mbaya" kutokana na idadi ya mauaji ya watu wengi kwa mwaka.

Visa hivyo viwili vimechangia idadi ya waathiriwa kutoka kwa visa vya mauaji ya halaiki ya mwaka huu hadi 197, pasi na kujumuisha wahalifu, rekodi nyingine tangu 2006, ripoti hiyo ilisema, ikiongeza kuwa watu wengine 91 walijeruhiwa katika ufyatuaji risasi.

Watu wakusanyika ndani ya Bunge la Jimbo la Tennessee katika kikao maalum kujadili usalama wa umma huko Nashville, Tennesse, Marekani.
Watu wakusanyika ndani ya Bunge la Jimbo la Tennessee katika kikao maalum kujadili usalama wa umma huko Nashville, Tennesse, Marekani.

Wataalamu wa masuala ya uhalifu Marekani walisema kuwa ongezeko la visa vya ufyatuaji risasi katika miaka iliyopita viliongeza wasiwasi kuhusu upatikanaji rahisi wa bunduki nchini humu.

Forum

XS
SM
MD
LG