Maandamano ya kuipinga Tume ya UN nchini humo, inayojulikana kama MONUSCO, yamezuka tangu Jumatatu na kusababisha vifo vya watu 19 ikiwemo walinda amani wa UN watatu.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Marekani Ned Price amesema, Marekani inatoa wito kwa taifa na mamlaka za ndani za DRC kuhakikisha ulinzi wa MONUSCO, maeneo yao na wanajeshi na waandamanaji kujieleza kwa njia ya amani.
Marekani imesema mashambulizi dhidi ya maafisa wa UN na maeneo yao ni kinyume cha sheria za kimataifa na inashukuru nia ya dhati ya DRC kuchunguza vitendo hivyo.