Sio chini ya watu watano wamepoteza maisha na wengine 12 kujeruhiwa Jumamosi katika mapigano makali kati ya Jeshi la Somalia na wapiganaji wa al-Shabab katika mkoa wa Bakol huko kusini magharibi ya Somalia, maafisa wamesema.
Maafisa wa jeshi la Serikali laSomalia wameiambia VOA kuwa wapiganaji walianzisha mashambulizi dhidi ya kambi ya kijeshi ilioko katika kijiji cha El Lahelay, kilichopo kilomita 20 magharibi ya makao makuu ya jimbo la Hudur.
Wapiganaji hao wakitumia bunduki aina ya machinegun na makombora yanayofurumusha mabomu walishambulia kutoka pande mbalimbali wakati wa mchana Jumamosi, wakivishambulia vikosi vya Somalia kwa silaha nzito kwa muda wa saa nzima, maafisa wamesema.
Walioshuhudia shambulizi hilo wameiambia VOA kwa sharti wasitajwe majina yao kuwa katika mkoa huo waliona miili angalau ya watu watano kutoka pande zote.
Wakati huohuo suluhu imefikiwa kati ya koo hasimu za wanamgambo walioko karibu na katikati ya mji wa Somalia, Beledweyne, kilomita 325 Kaskazini ya Mogadishu- hatua iliyokusudiwa kumaliza siku kadhaa za mapiganoambazo zimesababisha vifo vya watu wasiopungua 25.