Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:00

Shambulizi la kigaidi laua watu wanne Kenya


Wapiganaji wa al-Shabab
Wapiganaji wa al-Shabab

Bomu lililokuwa limetengenezwa kienyeji limeua watu wanne waliokuwa wanasafiri kwenye gari la abiria kaskazini ya Kenya katika kile kilichoelezwa kuwa inadhaniwa ni shambulizi la kigaidi,

Afisa wa serikali mmoja amesema Ijumaa, wakati wasiwasi wa ugaidi ukiendelea kusambaa kikundi cha msimamo mkali cha al-Shabab kilichoko Somalia kimeelezewa kuwa kimeamua kutumia mkakati mpya wa mashambulizi ya kinyama.

Mratibu wa kaskazini mashariki Mohamed Saleh amesema gari hilo lilikuwa na watu 15 na wengine 11 walikuwa wamejeruhiwa vibaya sana. Mmoja ya wale waliopoteza maisha ni chifu wa serikali na chifu mwengine alijeruhiwa vibaya sana, amesema Eric Oronyi, naibu kamishna wa kaunti. Gari hiyo ya abiria ilikuwa inatumika kibiashara katika njia ya Elwak-Mandera, amesema.

Mashambulizi kama hayo pia yametokea Kenya katika miezi iliyopita na kuuwa watu wasiopungua 34, wakiwemo maafisa wa polisi 20. Hata hivyo al-Shabaab wamedai kuhusika na mashambulizi hayo.

Kikundi hicho cha al-Qaida ambacho kinamafungamano na al-Shabab kimeahidi kulipiza kisasi Kenya kwa sababu nchi hiyo imepeleka vikosi vyake vya ulinzi Somalia tangia mwaka 2011 kupambana na ugaidi.

Kenya ni sehemu ya majeshi ya ushirika ya Umoja wa Afrika yaliyoko Somalia kuimarisha serikali ya nchi hiyo ambayo ni changa inayoendelea kushambuliwa na al-Shabab.

XS
SM
MD
LG