Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:17

Mali: Jeshi na wapiganaji wa Kiislamu washutumiwa kuua kiholela


Wanajeshi wa Mali.
Wanajeshi wa Mali.

Jeshi la Mali na makundi ya wapiganaji wa Kiislamu, yamefanya mauaji na kuhusika katika mamia ya visa vya ukiukaji wa haki za binadamu, Umoja wa Mataifa umesema katika ripoti mpya ambayo ina maelezo ya dhuluma dhidi ya raia.

Ripoti ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali (MINUSMA), iliyoonekana na AFP siku ya Alhamisi, inaorodhesha visa vya ukiukaji wa haki 375 nchini humo, kati ya mwezi Julai na Septemba, ikijumuisha visa 163 vinavyohusishwa na makundi ya wapiganaji wa Kiislamu 162 vinavyohusishwa na jeshi la Mali.

UN ilisema dhuluma hizo hazikuwa zimenakiliwa katika ripoti za awali.

Iliongeza kuwa visa 33 vilitekelezwa na wanamgambo, na 17 na vikundi vyenye silaha vilivyotia saini makubaliano ya amani ya 2015 kaskazini mwa Mali.

Ripoti inaeleza kwamba visa vingi vya ukiukaji wa haki za binadamu havikuripotiwa kwa sababu ya changamoto za msingi. Imeongeza kuwa Bamako imeanzisha uchunguzi.

Serikali ya Mali, ambayo ilichukua mamlaka mwaka 2020, mara nyingi inadai kuwa inafanya uchunguzi, lakini ni nadra kwa matokeo yake kuwekwa hadharani.

XS
SM
MD
LG