Ni hatua ya kutaka Iran ieleze chanzo cha chembechembe za madini ya uranium yaliyogundulika katika maeneo matatu, ripoti ya IAEA ya Alhamisi ambayo Reuters iliiona ilisema.
Hata hivyo Iran bado inasubiriwa kukabidhi mali ghafi mpya, na ombi lake lilikuja kabla ya mkutano wa wiki ijayo wa robo mwaka wa Bodi ya Magavana wa IAEA ambapo wanadiplomasia wanasema wanategemea mataifa ya Magharibi kushinikiza kutolewa azimio linaloitaka Iran kushirikiana, hatua ambayo Tehran kawaida haiifurahii.
“Shirika hilo limeisisitizia Iran kwamba katika mkutano huu linatarajia kuanza kupokea kutoka Iran maelezo ya kiufundi ya uhakika juu ya masuala haya, ikiwemo ruhusa ya kuingia katika maeneo mbalimbali na malighafi, na pia kuweza kuruhusiwa kuchukua sampuli inapohitajika kufanya hivyo,” moja ya ripoti mbili za siri za IAEA juu ya Iran zilizotumwa kwa nchi wanachama Alhamisi kabla ya mkutano huo wa bodi ilisema.
Suala hili la ukkosefu wa maelezo juu ya chembechembe za uranium limekuwa ni kikwazo cha upanuzi wa majadiliano haya ya kufufua makubaliano ya nyuklia ya Iran ya 2015 na mataifa yenye nguvu duniani, ilivyokuwa Tehran hivi sasa inataka uchunguzi wa IAEA ufungwe kama sehemu ya mazungumzo hayo, Mataifa yenye nguvu ya Magharibi yanasema.
Shirika la IAEA limesema haitaslimu amri kwa shinikizo la kisiasa na kazi yake ni kukagua malighafi zote za nyuklia. Malighafi hasa ambayo haijakabidhiwa inaelekea ilikuwepo katika maeneo hayo na hivyo ni lazima suala lifuatiliwe hadi kufikia ufumbuzi wake.