Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 14:58

Marekani itaangazia maandamano Iran katika kikao cha UN


Maandamano yenye ghasia yanaendelea Iran kufuatia kifo cha msichana Amini aliyefariki akiwa chini ya ulinzi wa polisi
Maandamano yenye ghasia yanaendelea Iran kufuatia kifo cha msichana Amini aliyefariki akiwa chini ya ulinzi wa polisi

Marekani na Albania zitafanya mkutano usio rasmi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatano, kulingana na barua inayoelezea tukio hilo, ambayo shirika la habari la Reuters imeiona

Marekani wiki ijayo itaangazia kwenye Umoja wa Mataifa juu ya maandamano nchini Iran yaliyochochewa na kifo cha msichana aliyekuwa chini ya ulinzi wa polisi na kutafuta njia za kuhamasisha uchunguzi wa kuaminika na huru kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu wa Iran.

Marekani na Albania zitafanya mkutano usio rasmi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatano, kulingana na barua inayoelezea tukio hilo, ambayo shirika la habari la Reuters imeiona. Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel raia wa Iran, Shirin Ebadi pamoja na mwigizaji na mwanaharakati mzaliwa wa Iran Nazanin Boniadi wanatarajiwa kutoa taarifa.

Mkutano huo utaangazia ukandamizaji unaoendelea wa wanawake na wasichana pamoja na wanachama wa makundi ya kidini na kikabila nchini Iran," ilisema barua hiyo. "Itabainisha fursa za kuhamasisha uchunguzi wa kuaminika na huru juu ya ukiukaji wa haki za binadamu na unyanyasaji uanofanywa na serikali ya Iran."

Mchunguzi huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Iran, Javaid Rehman, pia anatarajiwa kuhutubia mkutano huo ambao unaweza kuhudhuriwa na mataifa mengine wanachama wa Umoja wa Mataifa na makundi ya haki za binadamu.

XS
SM
MD
LG