Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 23:15

Makamu Rais wa Marekani Harris kuzuru Tanzania, Ghana na Zambia kuanzia Jumapili


Kamala Harris Selma Commemoration
Kamala Harris Selma Commemoration

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris anaanza ziara ya wiki moja barani Afrika mwishoni mwa wiki, wakati Marekani ikijaribu kujionyesha kama mshirika bora kuliko China, ambayo imewekeza fedha nyingi katika bara hilo kwa miongo kadhaa.

Harris atajadili ushiriki wa China katika masuala ya teknolojia na uchumi barani Afrika, ambayo yanaitia wasiwasi Marekani, pamoja na nafasi ya China katika urekebishaji wa madeni, maafisa waandamizi wa Marekani walisema.

Mojawapo ya nchi tatu ambazo Harris atazuru ni Zambia, ambayo ilikuwa nchi ya kwanza barani Afrika kutolipa deni lake kuu wakati wa janga la COVID-19, na inafanya kazi na wakopeshaji wake, pamoja na China, kufikia makubaliano.

Harris atakuwa Ghana kuanzia Jumapili hadi JumatanoMachi, kisha Tanzania kuanzia Machi Jumatano hadi Ijumaa, kabla ya kwelekea kituo chake cha mwisho ambacho ni Kituo chake cha mwisho ambacho ni Zambia, amabako atakuwa kuanzia Ijumaa hadi Jumamosi Aprili Mosi.

Atakutana na marais wa nchi hizo tatu na anapanga kutangaza uwekezaji katika sekta za umma na binafsi.

Afisa huyo, ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa sababu ya unyeti wa suala hilo, alisema Harris atajadili njia bora za jumuiya ya kimataifa kushughulikia changamoto za madeni zinazokabili Ghana na Zambia.

White House iliandaa Mkutano wa Viongozi wa Afrika mwezi Desemba, na Rais Joe Biden anatarajiwa kusafiri barani Afrika baadaye mwaka huu. Harris ana uhusiano wa kibinafsi na Zambia.

Babu yake mzaa mama alifanya kazi nchini humo, na alimtembelea huko akiwa msichana. Harris pia atakutana na viongozi vijana na wawakilishi wa biashara na kujadili mada kama vile mabadiliko ya hali ya hewa na uhaba wa chakula.

XS
SM
MD
LG