Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 10:12

Blinken na Kamala Harris wanahudhuria mkutano wa usalama Munich


Waziri wa mambo ya nje Marekani, Antony Blinken
Waziri wa mambo ya nje Marekani, Antony Blinken

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, mkuu wa NATO Jens Stoltenberg na mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa China Wang Yi watakuwa miongoni mwa wale watakaohudhuria mkutano huo wa kila mwaka

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anaanza ziara yake ya siku kadhaa barani Ulaya leo Ijumaa kwa kuhudhuria mkutano wa usalama mjini Munich. Pia atakwenda Uturuki na Ugiriki, kabla ya maadhimisho ya Februari 24 ya uvamizi wa Russia nchini Ukraine na wakati Uturuki ikiendelea na operesheni zake za uokoaji baada ya matetemeko makubwa ya ardhi kuleta uharibifu katika nchi hiyo mwanachama wa NATO wiki iliyopita.

Mkutano huo wa siku tatu wa usalama mjini Munich unafunguliwa Ijumaa. Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, mkuu wa NATO Jens Stoltenberg, na mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa China Wang Yi watakuwa miongoni mwa wale watakaohudhuria mkutano huo wa kila mwaka.

Mjini Munich, Blinken atashiriki katika mfululizo wa mikutano ya kujadili kuendelea kuiunga mkono Ukraine, na msaada kwa Uturuki na watu wa Syria baada ya matetemeko makubwa ya ardhi, wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema.

XS
SM
MD
LG