Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 19:01

Makampuni ya maji Uingereza yaamriwa kurudisha paundi milioni 114 kwa wateja


Wanaharakati wa maji taka wakati wa maandamano dhidi ya uchafuzi wa maji huko Brighton, Uingereza, Mei 20, 2023. Picha na Ben Stansall / AFP.
Wanaharakati wa maji taka wakati wa maandamano dhidi ya uchafuzi wa maji huko Brighton, Uingereza, Mei 20, 2023. Picha na Ben Stansall / AFP.

Mdhibiti wa Uingereza Jumanne aliamuru makampuni za maji nchini humo na Wales kurudisha jumla ya pauni milioni 114 kwa wateja kwa kushindwa kufikia malengo ya utendakazi, pamoja na uchafuzi wa mito.

Thames Water, msambazaji mkubwa nchini Uingereza, ambaye hivi karibuni alipata nyongeza ya pesa kutoka kwa wanahisa wakati wakijitahidi kuwa katika hali njema, kampuni hiyo ya maji iliamriwa kurudisha kiwango kikubwa sana cha paundi milioni 101.

Uamuzi wa mdhibiti wa maji Ofwat unakuja wakati kukiwa na kashfa ya muda mrefu kuhusu ubinafsishaji wa makampuni hayo ya maji yanayosukuma maji machafu kwenye njia za maji.

"Malengo tuliyoweka kwa makampuni yalitengenezwa ili kunyoosha -- kuendeleza uboreshaji kwa wateja na mazingira," mtendaji mkuu wa Ofwat David Black alisema katika taarifa.

"Hata hivyo, ripoti yetu ya hivi karibuni inaonyesha huduma imepungua, na kusababisha paundi milioni 114 kurejeshwa kwa wateja kwa kupunguziwa bili.

Mwezi Julai, Serikali ya Uingereza ilitangaza kampuni au mtu yeyote anayechafua mito nchini humo ambayo iko katika mifumo mingine ya ekolojia atatozwa faini isiyo na kikomo.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG