Ingawa hakuna uwekekano wa Israel kutii agizo hilo, amri hiyo itaongeza shinikizo kwa nchi kuzidi kutengwa.
Ukosoaji kwa vitendo vya Israel katika vita huko Gaza umeongezeka, hususan kuhusu operesheni zake huko Rafah— na hata kwa mshirika wake wa karibu Marekani.
Wiki hii peke yake , nchi tatu za Ulaya zimetangaza kuitambua Palestina kama taifa, na mwendesha mashtaka mkuu kwa mahakama nyingine ya Umoja wa Mataifa ameomba hati za kukamatwa kwa viongozi wa Israel, pamoja na maafisa wa Hamas.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu pia yuko katika shinikizo kali nyumbani ili kumaliza vita, ambavyo vilizuka wakati wanamgambo wa Hamas walipoingia ndani ya Israel, kuua watu 1,200 wengi wao raia na kuwachukua mateka watu wapatao 250.
Maelfu ya Waisrael kila wiki wamekuwa wakijumuika kufanya maandamano kuitaka serikali kufikia makubaliano na kuwarudisha nyumbani mateka nyumbani wakihofia kupoteza muda.
Forum