Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 02, 2025 Local time: 17:40

Rais Biden atupilia mbali wito wa Mahakama ya Kimataifa ya ICC


Rais wa Marekani Joe Biden aKIondoka Ikulu ya Marekani huko Washington, Marekani, kwa ajili ya kuchangisha fedha za kampeni huko California, Mei 9, 2024. (REUTERS).
Rais wa Marekani Joe Biden aKIondoka Ikulu ya Marekani huko Washington, Marekani, kwa ajili ya kuchangisha fedha za kampeni huko California, Mei 9, 2024. (REUTERS).

Rais wa Marekani Joe Biden siku ya Alhamisi alitupilia mbali wito wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa kutaka kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant,

Rais wa Marekani Joe Biden siku ya Alhamisi alitupilia mbali wito wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa kutaka kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant, pamoja na maafisa watatu wa ngazi za juu wa Hamas huko Gaza kwa tuhuma za uhalifu wa kivita kuhusiana na kipindi cha miezi saba cha mzozo.

Biden, katika mkutano wa waandishi wa habari huko White House, aliulizwa ikiwa Marekani ina ushahidi wowote kwamba Israel ilikuwa ikitumia njaa kwa wapalestina kama chombo cha vita kupambana na wanamgambo wa Hamas, kama mahakama ilivyodai wiki hii.

Biden hakujibu moja kwa moja lakini alisema, "Hatutambui mamlaka ya ICC jinsi inavyotekelezwa, ni hivyo tu."

Akizungumzia mwenendo wa vita, Biden, muungaji mkono wa muda mrefu wa Israel, alisema, "Hatufikirii kama kuna usawa kati ya kile Israel ilifanya na kile Hamas walichofanya.

Forum

XS
SM
MD
LG