Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 02:42

Maandamano yafanyika siku ya mwisho ya mkutano wa COP29

Vijana washinikiza haki za binadamu kuheshimwa kote duniani pembeni ya mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Hali ya Hewa huko Baku, Azerbaijan, Novemba 22, 2024.
Vijana washinikiza haki za binadamu kuheshimwa kote duniani pembeni ya mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Hali ya Hewa huko Baku, Azerbaijan, Novemba 22, 2024.

Makundi ya vijana yamelalamika pembeni ya mkutano wa Umoja wa Mataifa wa hali ya hewa uliofikia siku yake ya mwisho huko Baku, Aberzaijan, Ijumaa wakitoa wito wa kuheshimiwa haki za binadamu kote duniani.

Geogina Kerubo wa kundi la Global Young Green anasema ni jukumu lao kama wanaharakati kuwaelimisha watu juu ya masuala ambayo ni muhimu yanayowahusu.

Maandamano yamefanyika wakati wajumbe wamekuwa wakijadili pendekezo kutoka nchi zilizoendelea kuongeza kiwango cha kugharimia athari za mabadiliko ya hali ya hewa kufikia dola bilioni 250 kutoka bilioni 100.

Viongozi wanawake wakiwa katika picha ya pamoja katika mkutano wa COP29, Alhamisi, Novemba 21, 2024, Baku, Azerbaijan.
Viongozi wanawake wakiwa katika picha ya pamoja katika mkutano wa COP29, Alhamisi, Novemba 21, 2024, Baku, Azerbaijan.

Hata hivyo mataifa yanayoendelea wanasema kiwango hicho hakitoshi wakati wanahitaji hivi sasa dola trilioni 1.3 kugharimia athari hizo kufikia 2035.

Forum

XS
SM
MD
LG