Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 00:16

Maandamano yafanyika New Zealand dhidi ya masharti ya chanjo


Waziri Mkuu Jacinda Ardern
Waziri Mkuu Jacinda Ardern

Maelfu ya watu wameandamana katika mji mkuu wa New Zealand, Wellington, Alhamisi, kupinga masharti ya chanjo ya COVID-19 na kufungwa kwa shughuli.

Upingaji huo unajiri wakati nchi ikiwa imefikia kiwango cha kihistoria cha kuwapatia chanjo kamili takriban asilimia 90 ya watu wake.

Waandamanaji, wengi wao wakiwa hawana barakoa waliingia katikati ya wilaya ya kibiashara huko Wellington na kukusanyika mbele ya jengo la bunge maarufu kama Beehive.

Usalama uliongezwa nje ya bunge huku milango ya kuingilia ndani ikiwa imezibwa na dazeni ya polisi waliopelekwa huko.

Chini ya shinikizo kali, Waziri Mkuu Jacinda Ardern alilegeza masharti mengi kabla ya kipindi cha msimu wa Krismas na kuachana na mkakati wa muda mrefu wa kutokomeza virusi vya corona kwa ajili ya mfumo wa kuishi na virusi kwa kuhakikisha watu wengine zaidi wanapatiwa chanjo.

Serikali ilitoa maagizo kwa waalimu, wafanyakazi katika sekta za afya, na sekta za walemavu, polisi na sekta nyingine za umma kuhakikisha wanapatiwa chanjo.

XS
SM
MD
LG