Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 12:32

Auckland kubaki katika masharti makali kudhibiti milipuko ya virusi vya Delta


Waziri Mkuu Jacinda Ardern
Waziri Mkuu Jacinda Ardern

Waziri Mkuu wa New Zealand ametangaza Jumatatu kwamba mji mkubwa zaidi nchini humo, wenye wakazi milioni 1.7, utabaki katika masharti makali au kufunga shughuli ikiwa ni juhudi za kuzuia milipuko midogo midogo ya virusi vya Delta vinayoambukiza sana.

"Ni wazi kuwa hakuna maambukizi makubwa ya virusi huko Auckland," Waziri Mkuu Jacinda Ardern alisema, "lakini kwa vile tuna kesi mpya zinazoibuka, kuna hatari," amesema kwenye mkutano wa waandishi wa habari.

Kufungwa kwa Auckland kumeongezwa hadi Septemba 21, na kesi mpya 33 zilirekodiwa Jumatatu, kufuatia ripoti za mwishoni mwa juma za kesi 23 na 20.

New Zealand iliweka masharti kote nchini Agosti 17. Baadhi ya vizuizi, viliruhusu watu kurudi ofisini na shule, viliondolewa katika maeneo mengine huko New Zealand wiki iliyopita.

Wakati huo huo Israeli ilionya kuwa wasafiri kutoka nchi hiyo waliokwenda mji wa Uman wa Ukraine kwa ajili ya sherehe za Rosh Hashanah na kurejea tena Israeli huku wakiwa na vyeti vya kugushi vya matokeo ya COVID watakabiliwa na mashtaka kamili ya jinai.

Serikali ya Israeli inaangalia kwa umakini mkubwa suala la wagonjwa kuingia Israeli kwa ulaghai kwa kughushi nyaraka ”ofisi ya Waziri Mkuu Naftali Bennett ilisema katika taarifa yake.

XS
SM
MD
LG