Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 14:14

Maafisa wawahimiza wakazi kuchukua tahadhari baada ya kimbunga Hilary kupiga Los Angeles


Picha ya Satellite zikionyesha ukubwa wa kimbunga Hilary kilichopiga huko California. Picha na (NOAA kupitia AP)
Picha ya Satellite zikionyesha ukubwa wa kimbunga Hilary kilichopiga huko California. Picha na (NOAA kupitia AP)

Kimbunga cha kwanza kupiga Los Angeles baada ya zaidi ya miaka 80 kimesababisha mafuriko kwenye maeneo ya kusini mwa California ambayo kwa kawaida yamezoeleka kwa  ukame wakati maafisa wakiwahimiza watu kuwa  salama wakati wanapoanza kuhesabu gharama ya uharibifu.

Meya wa Los Angeles Karen Bass amesema bado alikuwa na wasiwasi kwamba watu wanaweza kujisahau kama kimbunga Hilary kimewaacha bila ya madhara makubwa, lakini baadae dhoruba inaweza kurejea tena na kuwashangaza watu ambao hawakujitayarisha.

Matope na miamba iliangukia kwenye barabara kuu, huku maji yakifurika kwenye barabara na matawi ya miti kuanguka katika maeneo jirani kuanzia San Diego hadi Los Angeles.

Gari ikipita katika eneo lililofurika maji baada ya kimbunga Hilary kutua katika eneo la Palm Springs, California Aug. 20, 2023.
Gari ikipita katika eneo lililofurika maji baada ya kimbunga Hilary kutua katika eneo la Palm Springs, California Aug. 20, 2023.

Dazeni ya magari yalikwama kwenye maji ya mafuriko katika eneo ambalo kwa kawaida lina joto na hali ya ukavu huko Palm Desert na kwenye jamii zinazozunguka kwenye bonde la Coachella.

Video kutoka televisheni ya KESQ zilionyesha magari yakipita kwenye mitaa yenye mafuriko huko Palm Springs. Wafanyakazi walikuwa wakitoa maji ya mafuriko kutoka kwenye chumba cha dharura katika kituo cha afya cha Eisenhower huko Rancho Mirage.

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali.

Forum

XS
SM
MD
LG