Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 03:54

Maafisa wa NATO na Ukraine kujadili kampeni za kivita za Russia dhidi ya Ukraine


Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg
Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg

Maafisa wa NATO na Ukraine wanatarajiwa kukutana wiki ijayo kujadili kampeni ya mashambulizi ya anga ya Russia dhidi ya Ukraine, ambayo yamehusisha wimbi kubwa la mashambulizi tangu kuanza mwaka 2024.

Msemaji wa NATO Dylan White alisema Alhamisi kuwa Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg ataitisha mkutano wa Baraza la NATO na Ukraine Januari 10 “kufuatia mashambulizi ya makombora na droni yanayofanywa na Russia.”

Ukraine imewashinikiza washirika kuimarisha ulinzi wa anga wa nchi hiyo, wakati Russia kila siku imetumia makombora na droni kufanya mashambulizi yanayoilenga miji ya Ukraine.

Mashambulizi ya Russia mawili ya usiku yaliyokuwa ya nguvu zaidi yamefanyika wiki mbili zilizopita, ikiwemo darzeni za makombora na droni zilizoulenga mji mkuu, Kyiv.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba alisema Jumatano kuwa suala muhimu la mkutano wa Baraza la NATO na Ukraine itakuwa kuimarisha ulinzi wa anga wa Ukraine, na alitaja mazungumzo hayo kuwa “ni ishara muhimu ya mshikamano wa nchi za Ulaya na Atlantic katika kukabiliana na ongezeko la tishio la Russia.”

Siku ya Jumanne, Kuleba aliwataka washirika kuharakisha kupeleka mifumo ya ulinzi wa anga na silaha Ukraine, na kuyapatia majeshi ya Ukraine droni za kivita na makombora ya masafa marefu yanayoweza kusafiri zaidi ya kilomita 300.

Kuleba pia alitaka idhini itolewe kutumia mali za Russia zilizokamatwa ili kuisaidia Ukraine na kuwatenga wanadiplomasia wa Russia.

Ukraine ilisema Alhamisi kuwa Russia iliendeleza mashambulizi ya anga usiku kucha na droni mbili ambazo ulinzi wa anga wa Ukraine ulizitungua katika eneo la Khmelnytskyi.

Shambulizi la Russia lilihusisha makombora matatu ya masafa marefu yaliyoilenga kharkiv na Donetsk, jeshi la anga la Ukraine lilisema.

Baadhi ya taarifa katika ripoti hii inatokana na mashirika ya habari ya AFP na Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG