Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:55

Milipuko na Moshi yatanda Kyiv wakati Russia ikifanya mashambulizi makubwa


Athari ya shambulizi la anga lililofanywa na Russia katika mji wa Kyiv.
Athari ya shambulizi la anga lililofanywa na Russia katika mji wa Kyiv.

Russia imeshambulia kwa kutumia makombora tofauti wakati wa majira ya asubuhi yaliyokuwa na harakati nyingi, wakipiga majengo ya waakaazi  na miundombinu ya raia.

Rais wa Russia Vladimir Putin
Rais wa Russia Vladimir Putin

Mamlaka za jeshi zilitoa onyo la mashambulizi ya anga ambalo lilidumu kwa saa tatu.

Shambulizi limekuja saa kadhaa baada ya rais wa Russia Vladmir Putin kusema shambulizi la anga katika mji wa Russia – Belgorod, halitapita bila kuadhibiwa. Moscow imesema shambulizi la anga limeuwa raia 24 na kuilaumu Ukraine.

Meya wa Kyiv Vitali Klitschiko amesema mwanamke mzee alikuwa katika gari la kubeba wagonjwa baada ya kujeruhiwa. Awali alisema kwamba takriban watu 16 wamejeruhiwa katika mji mkuu.

Mabomba yameharibiwa katika wilaya ya Pecherskyi huko Kyiv , na umeme na maji vimekatwa katika wilaya mbalimbali za mji mkuu.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG