Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 22:57

Maadamano ya kutaka wafungwa wa kisiasa kuachiliwa yafanyika Tunisia


Raia wa Tunisia wakibeba mabango wakati wa maandamano mjini Tunis kutaka wafungwa wa kisiasa kuachiliwa huru.
Raia wa Tunisia wakibeba mabango wakati wa maandamano mjini Tunis kutaka wafungwa wa kisiasa kuachiliwa huru.

Mamia ya wafuasi wa muungano mkuu wa upinzani nchini Tunisia Jumapili waliandamana kutaka takriban watu 20, ikiwa ni pamoja na wapinzani wa rais Rais Kais Saied, kuachiliwa huru.

Takriban waandamanaji 300, wengi wakiwa na picha za wale waliowaita "wafungwa wa kisiasa," walikusanyika katikati mwa mji mkuu, Tunis, kuwatetea mawaziri wa zamani, wafanyabiashara na wengine ambao wamelkuwa wkizuiliwa tangu mwezi Februari mwaka huu.

Mwezi Machi Bunge la Ulaya, katika azimio lisilo na uzito wa kisheria, lilishutumu "msimamo" wa Saied, ambaye anasema waliozuiliwa walikuwa "magaidi" waliohusika katika "njama dhidi ya usalama wa serikali".

Tunisia ilikuwa ni demokrasia pekee iliyoibuka kutokana na machafuko ya Arab Spring katika eneo hilo zaidi ya muongo mmoja uliopita, lakini Saied mnamo Julai 2021, alisimamisha, kisha kulivunja bunge, kama sehemu ya unyakuzi wa madaraka uliomruhusu kutawala kwa amri za kiutendaji.

"Uhuru! Uhuru!" waandamanaji waliimba, pia wakitaka uchaguzi ufanyike kabla ya tarehe iliyopangwa ya Oktoba mwaka 2024.

Miongoni mwa waliozuiliwa ni Rached Ghannouchi, mkuu wa chama chenye msukumo wa Kiislamu cha Ennahdha, ambacho kilikuwa kikubwa zaidi bungeni, kabla ya Saied kunyakua madaraka.

Forum

XS
SM
MD
LG