Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 02:21

Jaji nchini Tunisia apiga marufuku vyombo vya habari kuripoti kesi za wapinzani


Rais wa Tunisia Kais Saied
Rais wa Tunisia Kais Saied

Jaji mmoja nchini Tunisia amepiga marufuku vyombo vya habari nchini humo kuripoti kuhusu kesi za wapinzani wanaoshutumiwa kupanga njama dhidi ya usalama wa taifa katika miezi ya hivi karibuni, shirika la habari la serikali TAP limesema Jumamosi.

Amri hiyo imezua wasiwasi juu ya haki nchini Tunisia tangu Rais Kais Saied aliponyakua madaraka yote mwaka 2021, akitawala kwa amri ya kiutendaji na kujipa mamlaka ya mahakama.

msemaji wa mahakama hiyo Hanan el-Qadas ameiambia TAP kwamba “Ofisi ya Jaji inayofanya uchunguzi ya tawi la kupambana na ugaidi imetoa uamuzi unaopiga marufuku vyombo vya habari kutangaza kesi mbili za kupanga njama dhidi ya usalama wa taifa, “.

Majaji waliwaweka kizuizini au kufungua uchunguzi dhidi ya zaidi ya watu mashuhuri 20 kutoka sekta ya siasa, mahakama, vyombo vya habari na biashara wenye uhusiano na upinzani katika miezi ya hivi karibuni, wakiwashtumu baadhi yao kupanga njama dhidi ya usalama wa taifa.

Vyama vikuu vya upinzani vilikisoa vikali kukamatwa kwa watu hao kuwa ni hatua iliyochochewa na siasa, nayo mashirika ya kutetea haki za binadamu yamezitaka mamlaka za Tunisia kuwaachilia huru wanaozuiliwa.

Forum

XS
SM
MD
LG