Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 22:55

Umoja wa Ulaya unafikiria kuisaidia Tunisia Euro bilioni moja


Ursula von der Leyen, Mkuu wa Tume ya Ulaya
Ursula von der Leyen, Mkuu wa Tume ya Ulaya

Nchi hiyo ya Afrika Kaskazini, yenye deni kubwa ipo katika mazungumzo ya mkopo wa IMF imekuwa lango kuu la wahamiaji na wale wanaotafuta hifadhi wanaojaribu kufanya safari hatari za kwenda Ulaya

Umoja wa Ulaya umesema Jumapili kwamba unafikiria kutoa usaidizi zaidi ya euro bilioni moja ili kuimarisha uchumi wa Tunisia na kupunguza wimbi la wahamiaji wasio wa kawaida wanaovuka bahari ya Mediterania.

Nchi hiyo ya Afrika Kaskazini, yenye deni kubwa ipo katika mazungumzo ya mkopo wa IMF, imekuwa lango kuu la wahamiaji na wale wanaotafuta hifadhi wanaojaribu kufanya safari hatari za kwenda Ulaya.

EU iko tayari kuipatia Tunisia Euro milioni 900 katika misaada ya muda mrefu pamoja na euro milioni 150 kwa msaada wa haraka katika jitihada za kuimarisha uhusiano wetu, mkuu wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen alisema akiwa katika ziara ya pamoja na mawaziri wakuu wa Italy na Uholanzi.

Msaada huo utategemea idhini ya mkopo wa karibu dola bilioni 2 ambao kwa sasa unajadiliwa na Shirika la Fedha la Kimataifa kulingana na hati iliyowekwa kwenye tovuti ya Tume ya Ulaya.

Forum

XS
SM
MD
LG