Ajali hiyo ilitokea Jumatatu jioni wakati wafanyakazi katika mgodi uliopo Kaskazini mwa jiji la Rustenburg. Wafanyakazi wote waliojeruhiwa walilazwa hospitali.
Mtendaji Mkuu wa waendesha mgodi wa Mine Operator Impala Platinum Holdings Nico Muller amesema katika taarifa yake kuwa ilikuwa "siku ya giza kubwa katika historia ya Implats." Alisema uchunguzi umeanza kubaini kilichosababisha lifti hiyo kushuka na mgodi huo ulisimamisha shughuli zote siku ya Jumanne.
Waziri wa Rasilimali Madini na Nishati Gwede Mantashe alisema serikali itafanya uchunguzi kuhusiana na janga hilo baya. Aliutembelea mgodi huo na kupewa taarifa, serikali ilisema.
Wafanyakazi wote 86 waliouawa au kujeruhiwa walikuwa kwenye lifti, msemaji wa Implats Johan Theron alisema.
Baadhi ya waliojeruhiwa walikuwa "wamevunjika mifupa," alisema. Theron alisema lifti hiyo ilidondoka takriban mita 200, pamoja hayo yalikuwa makadirio ya awali. Aliita ajali isiyo ya kawaida kabisa.
Lifti hiyo kubwa ina ngazi tatu, kila moja ikiwa na uwezo wa kuchukua wafanyikazi 35, Implats ilisema. Shimo la mgodi lina takriban kilomita moja.
Afrika Kusini ndiyo mzalishaji mkubwa zaidi wa platinam duniani. Mgodi wa Impala Rustenburg una mashimo tisa na ulikuwa mgodi mkubwa zaidi wa platinamu kwa uzalishaji mwaka jana.
Forum