Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 17, 2024 Local time: 19:39

Liberia wapigakura kumchagua rais


Maafisa wa kituo cha kupigia kura wakilinganisha hati ya kitambulisho cha mpiga kura na taarifa katika daftari la wapiga kura huko Monrovia mnamo Novemba 14, 2023.Picha na RAMI BALAGHI / AFP
Maafisa wa kituo cha kupigia kura wakilinganisha hati ya kitambulisho cha mpiga kura na taarifa katika daftari la wapiga kura huko Monrovia mnamo Novemba 14, 2023.Picha na RAMI BALAGHI / AFP

Raia wa Liberia wameanza kupiga kura mapema Jumanne katika uchaguzi wa marudio kati ya rais George Weah na makamu wa rais wa zamani Joseph Boakai ambao walikuwa wamekaribiana sana katika duru ya kwanza lakini hawakupata asilimia 50 zilizohitajika kupata ushindi.

Mchezaji wa zamani wa soka, weah alipata asilimia 43.83 ya kura dhidi ya Boakai aliyepata asilimia 43.44 ikiwa wamepishana kidogo sana jambo ambalo limezusha matarajio ya kuwa na ushindani mkali katika duru ya pili .

Mwandishi wa habari wa shirika la Reuters alishuhudia mistari mirefu katika vituo vya kupigia kura kwenye mji mkuu wa Monrovia.

Rais aliyoko madarakani Weah aliwaomba wapiga kura muda zaidi ili kutekeleza ahadi zake alizozitoa katika muhula wake wa kwanza, ikiwemo kuondoa rushwa na kuboresha maisha ya watu.

Taifa hilo la afrika magharibi bado linapambana na vita viwili vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka 1989 na 2003 na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola wa mwaka 2013 hadi mwaka 2016 ambao ulisababisha vifo vya maelfu ya watu.

Wote Weah na Boakai wamepata uungwaji mkono kutoka kwa wagombea wengine waliopoteza katika duru ya kwanza ya uchaguzi.

Forum

XS
SM
MD
LG