Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 12:27

Duru ya pili ya uchaguzi Liberia ni Rais George Weah na mpinzani Joseph Boakai


Rais wa Liberia aliyepo madarakani George Weah (R) na mpinzani wake mkuu Joseph Boakai (L). Picha na JOEL SAGET na Brendan SMIALOWSKI / AFP.
Rais wa Liberia aliyepo madarakani George Weah (R) na mpinzani wake mkuu Joseph Boakai (L). Picha na JOEL SAGET na Brendan SMIALOWSKI / AFP.

Ni mara ya pili kwa Boakai kugombea nafasi ya juu tayari alishindwa na Rais George Weah katika duru ya pili ya uchaguzi 2017. Wawili hao wanakabiliana tena katika duru ya pili ya uchaguzi siku ya Jumanne kufuatia uchaguzi wa kwanza wa mwezi uliopita ambapo hakuna aliyepata ushindi wa moja kwa moja

Mgombea mkuu wa upinzani nchini Liberia anayewania urais, Joseph Boakai ana uzoefu wa kisiasa wa miongo minne, lakini akiwa na umri wa miaka 78 anakabiliwa na changamoto ya kushinda idadi kubwa ya vijana.

Alikuwa Makamu wa Rais kuanzia mwaka 2006 hadi 2018 kwa Ellen Johnson Sirleaf, Rais wa kwanza mwanamke barani Afrika ambaye aliijenga upya Liberia iliyoharibiwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyopelekea vifo vya watu 250,000.

Hii ni mara ya pili kwa Boakai kugombea nafasi ya juu, tayari alishindwa na Rais George Weah katika duru ya pili ya uchaguzi mwaka 2017. Wawili hao wanakabiliana tena katika duru ya pili ya uchaguzi siku ya Jumanne kufuatia uchaguzi wa kwanza wa mwezi uliopita ambapo hakuna aliyepata ushindi wa moja kwa moja.

Boakai amevunja rekodi ya mpinzani wake, mchezaji nyota wa zamani wa kimataifa na kusisitiza uzoefu wake ofisini akipendekeza “mpango wa kuiokoa” nchi hiyo ya Afrika Magharibi. Ameahidi kuboresha miundombinu, kuwekeza katika kilimo, kuvutia uwekezaji, kuifungua nchi kwa utalii na kurejesha sifa ya Liberia.

Forum

XS
SM
MD
LG