Picha ya setilaiti kuanzia Agost 5, ilichukuliwa na Planet Labs imeonyesha eneo la kivuko kilichopo kati ya jiji la Kaesong la Korea ya Kaskazini la na jiji la Paju la korea ya Kusini.
Shirika la habari la Reuters halikuweza kusibitisha lenyewe maeneo ambayo yaliyo sitishwa, lakini picha zilizopigwa siku ya tarehe tano mwezi Agost mwaka 2024 zinaonyesha moja ya barabara zinaziunganisha Korea ya Kusini na Kaskazini mpakani.
Tangazo hilo linaashiria ongezeko zaidi la shughuli katika eneo la jirani kwenye mpaka unaozitenganisha nchi hizo mbili za Korea.
Korea ya Kaskazini imeanza kuweka mabomu ya ardhini na vizuizi na kutengeneza eneo la taka pembeni mwa mpaka wenye majeshi kwa miezi kadhaa mwaka huu mbali na ajali, jeshi la Korea ya Kusini limesema mwezi Julai.
UNC inayoongozwa na Marekani ni kikosi cha kijeshi cha Kimataifa na inasimamia masuala katika eneo lisilo na jeshi (DMZ) kati ya nchi hizo mbili za Korea.
Forum