Shirika la habari la serikali ya Korea Kaskazini, KCNA limeripoti kwamba, “nchi itaendelea kuboresha mkakati wake wa uimara katika kila nyanja, na kuondoa aina yoyote ya changamoto za kiusalama ambazo zitakuwa ni matokeo ya mpango uliopitiwa upya wa Washington.”
Gazeti la New York Times wiki hii liliripoti kwamba mpango wa Marekani uliopitishwa na Rais Joe Biden, mwezi Machi, ulikuwa kwa ajili ya kuandaa uwezekano wa uratibu wa kukabiliana na Russia, China, na Korea Kaskazini.
Mpango huo ambao ni siri kubwa kwa mara ya kwanza unaeleza mpango wa kimkakati wa Washington, kujikita kwa kukabiliana na upanuzi mkubwa wa program ya silaha za nyuklia za China, kwa mujibu wa gazeti la The New York Times.
Forum